Umoja ni Nguvu
Tuungane Kusaidiana

JamiiSafe ni kikundi cha Kitanzania cha kusaidiana ambapo wanachama wanachangia kila mwezi ili kupata msaada wa kifedha wakati wa ugonjwa au msiba. Jiunge nasi na uhakikishe usalama wa familia yako.

0+
Wanachama
3
Viwango vya Michango
24/7
Msaada wa Jamii
Viwango vya Kunufaika

Unapata Nini Unapokuwa na Shida?

Kila mwanachama anayechangia kwa wakati atapata msaada wa kifedha kulingana na kiwango chake wakati wa ugonjwa au msiba. Fedha zinagawanywa kulingana na aina ya msaada.

Msingi
10,000 Tsh/mwezi
Changia kidogo, pata msaada mkubwa wakati wa shida!
Wakati wa Ugonjwa
Tsh 200,000
Wakati wa Msiba
Tsh 500,000
  • Msaada wa matibabu ya dharura
  • Gharama za mazishi za msingi
  • Usafirishaji wa msiba
Jiunge Msingi
Juu
100,000 Tsh/mwezi
Ulinzi KAMILI kwa familia yako nzima!
Wakati wa Ugonjwa
Tsh 2,000,000
Wakati wa Msiba
Tsh 5,000,000
  • Msaada wa matibabu wa juu
  • Gharama za mazishi kamili
  • Msaada wa familia kwa miezi
  • Huduma za ziada za msaada
ULINZI KAMILI - Familia Nzima!
Jiunge Juu
Jinsi Inavyofanya Kazi

Hatua 4 Rahisi za Kujiunga

Kujiunga na JamiiSafe ni rahisi sana. Fuata hatua hizi na uwe sehemu ya jamii yenye nguvu.

Jisajili Mtandaoni

Fungua akaunti yako kwa kujaza fomu ya usajili pamoja na picha yako na kuchagua kiwango chako.

Thibitishwa na Admin

JamiiSafe itathibitisha ombi lako na mwanachama rasmi wa JamiiSafe, kwa kupokea sim au ujumbe mfupi kupitia namba yako.

Changia Kila Mwezi

Changia kiasi chako kila mwezi taratibu au fedha yote. kiwango chako kitadhibitishwa mchango wako na utaonekana kwenye profile yako.

Pata Msaada Unapohitaji

Wakati wa Mgonjwa au Msiba, Jamii Safe inakusaidia kifedha kulingana na kiwango chako.

Muhtasari wa Viwango

Linganisha Viwango Vyote

Tazama kiasi utakachopata kutoka JamiiSafe wakati wa shida kulingana na kiwango chako. Fedha zinagawanywa kwa aina ya msaada.

Kundi Mchango Ugonjwa Msiba
Msingi Tsh 10,000 Tsh 200,000 Tsh 500,000
Wastani Tsh 50,000 Tsh 1,000,000 Tsh 2,500,000
Juu Tsh 100,000 Tsh 2,000,000 Tsh 5,000,000

* Mchango ni wa kila mwezi. Unapata msaada wa ugonjwa AU msiba kulingana na hali yako.

Kwa Nini JamiiSafe?

Faida za Kujiunga Nasi

JamiiSafe si tu kikundi - ni familia inayokusaidia wakati wa shida kubwa zaidi.

Umoja wa Jamii

Kuwa sehemu ya jamii inayojali na kusaidiana. Kila mwanachama ni muhimu na anapendwa katika JamiiSafe.

Usalama wa Familia Yako

Michango yako midogo kila mwezi inahakikisha utapata msaada mkubwa wakati unaohitaji zaidi.

Uwazi Kamili

Kila mchango unaonekana kwenye profile yako. Admin anadhibitisha na wewe unaona kiasi chako kila wakati.

Wanachama Wanasema

Hadithi za Mafanikio

Sikiliza kutoka kwa wanachama wenzetu ambao JamiiSafe imewasaidia wakati wa shida.

Nilipougua na kuhitaji upasuaji wa dharura, JamiiSafe walinisaidia na dawa (Tsh 800,000) na gharama za upasuaji (Tsh 1,000,000). Sikupewa fedha zote mkononi - zilienda moja kwa moja hospitalini. Asante sana!

Mwanachama wa JamiiSafe

Mama Zawadi

Mwanachama wa Kiwango cha Wastani

Wakati wa msiba wa baba yangu, JamiiSafe ilitoa msaada wa usafirishaji (Tsh 500,000), gharama za mazishi (Tsh 1,500,000) na msaada wa familia (Tsh 500,000). Jumla Tsh 2,500,000 ndani ya siku 2!

Mwanachama wa JamiiSafe

Bwana Juma

Mwanachama wa Kiwango cha Wastani
Maswali na Majibu

Maswali Yanayoulizwa Zaidi

Pata majibu ya maswali yako kuhusu JamiiSafe na jinsi inavyofanya kazi.

JamiiSafe ni kikundi cha kusaidiana ambapo wanachama wanachangia kiasi fulani kila mwezi. Fedha zinazokusanywa zinatumika kusaidia wanachama wakati wa ugonjwa au msiba. Ukiwa mwanachama hai na ukachangia kwa wakati, utapata msaada wa kifedha kulingana na kiwango chako wakati unapohitaji.

Kuna viwango vitatu unaweza kuchagua:
Msingi: Tsh 10,000/mwezi - Ugonjwa: 200,000, Msiba: 500,000
Wastani: Tsh 50,000/mwezi - Ugonjwa: 1,000,000, Msiba: 2,500,000
Juu: Tsh 100,000/mwezi - Ugonjwa: 2,000,000, Msiba: 5,000,000

Baada ya kujiunga na kuthibitishwa na Admin, unahitaji kuchangia kwa angalau miezi 3 mfululizo kabla ya kuwa na haki ya kupata msaada. Hii inasaidia kuhakikisha uendelevu wa mfuko na uaminifu kati ya wanachama.

Ukipata ugonjwa au msiba, wasiliana na Admin kupitia WhatsApp: +255 670 711 791. Admin atakagua hali yako na kuidhinisha msaada kulingana na kiwango chako. Fedha zinatolewa kulingana na mahitaji halisi - kwa mfano, dawa hulipwa moja kwa moja hospitalini.

Ndiyo! Michango yote inahifadhiwa kwa uaminifu na unaona historia yako yote kwenye profile yako. Admin anadhibitisha kila mchango na unaona kiasi chako kila wakati. JamiiSafe inafanya kazi kwa uwazi kamili - hakuna fedha zinazofichwa.

Ndiyo, unaweza kuomba kubadilisha kiwango chako kwa kuwasiliana na Admin. Ukipanda kiwango (mfano kutoka Msingi kwenda Wastani), utaanza kupata faida za kiwango kipya baada ya miezi 3 ya kuchangia kwa kiwango kipya.

Ukiacha kuchangia kwa zaidi ya miezi 2 mfululizo bila sababu ya msingi, utapoteza haki ya kupata msaada hadi utakaporudi kuchangia tena kwa miezi 3 mfululizo. Michango uliyotoa awali haibailiwi - imesaidia wanachama wengine wakati wa shida zao.

Wanachama wa JamiiSafe wakisaidiana

Jiunge na JamiiSafe Leo!

Usikae peke yako wakati wa shida. Jiunge na jamii ya watu wanaojali na tuungane kusaidiana. Changia kidogo, pata msaada mkubwa wakati unaohitaji zaidi.

Jiunge Sasa - Bure Kujisajili